Published - Thu, 01 Dec 2022

MATOKEO YA DARASA LA SABA 2022

MATOKEO YA DARASA LA SABA 2022

Baraza la mitihani Tanzania limetangaza matokeo ya mtihani wa kumaliza darasa la saba yaani Primary school leaving examination (PSLE) mwaka 2022

Bonyeza hapa ili uone matokeo hayo

Matokeo ya darasa la saba 2022

Created by

Dr. Mlelwa

Dr. Mlelwa is an experienced online tutor in biology and chemistry from ordinary level to advanced level. His highest level of education is two years of doctor of medicine (MD) at Muhimbili university of Health and allied science in from Nov 2018 to Sept 2020. There after he failed to continue with Doctor of Medicine Studies due to several reasons which are out of scope of this description. He started online teaching since January 2020 in his YouTube channel (Dr.Mlelwa Lectures) by that time he was still a medical student dreaming to become one among the best tutor in medical studies, that's why he called the channel Dr. Mlelwa Lectures, comparing to Dr. Najeeb Lectures who was one of his role mode. His good performance, being the second best boy in advanced biology examinations national wise in 2018, made him one among most interesting online tutor, having influence to different students inside Tanzania as well as abroad.

Naitwa Helbeth Issack Mlelwa. Siku ya ijumaa, March 13, 1998, historia na kumbukizi za wazazi wangu zinasema kwamba ndio siku ambayo nilizaliwa na nafsi yangu ikaonja pumzi ya duniani. Kwa kuwa wazazi wangu walikuwa wakatoliki, walitumia vitabu vya kalenda za kikatoliki vinavyoitwa shajara kuangalia jina la mtakatifu wa siku hiyo ndio liwe jina langu. Jina la mtakatifu wa siku hiyo likawa ni Herberth (lenye asili ya kijerumani na maana yake ni BRIGHT ARMY, yaani jeshi lenye akili) ambalo baadae walishindwa kuliandika sawa sawa kwenye nyaraka za kielimu ndio likaenda kuwa Helbeth. Matamshi ya jina yanafanana, ijapokuwa silabi zinatofautiana.

Mwaka 2004 nilianza masomo yangu ya awali, shule ya msingi Lilondo, kata ya wino, tarafa ya madaba iliyoko wilayani Songea vijijini (mahali nilikozaliwa). Kutoka naanza awali mpaka nafika darasa la saba, mara nyingi nilishika nafasi ya kwanza au ya pili darasani. Wakati huo mwalimu wetu mkuu alikuwa anaitwa Mwingira ambaye alifariki wakati tunaelekea kuhitimu darasa la saba na kuletwa mwalimu Magulukwivala Mwenda aliyetokea shule ya msingi Wino. Baadhi ya waalimu wangu ninaowakumbuka ni pamoja na Mwl Dwigo (kiingereza), Mwl. Mkinga (hesabu), Mwl. Kiyao (uraia), Mwl. Wella (Jografia), Mwl.  Nolsensia Mwenda, maarufu kwa jina la samwenda (sayansi), Mwl. Felister Mlelwa, maarufu kwa jina la mwalimu F, (kiswahili), Mwl. Kipera (kiswahili na uraia), Mwl. Medard Mlelwa, maarufu kwa jina la "tilia maanane" yaani sikiliza kwa umakini ninapofundisha (historia) na waalimu wengine sikumbuki hata masomo yao

Mwaka 2011, nilimaliza darasa la saba na 2012 nikaanza kidato cha kwanza katika shule ya Wino sekondari iliyoko Songea Vijijini. Maendeleo yangu ya kitaaluma yaliendelea kuwa bora hata katika shule ya Wino sekondari pamoja na ugumu wa mazingira, uhaba wa waalimu wa kutosha hata katika masomo ya sayansi na upatikanaji wa vitabu vya kutosha. Nafasi yangu darasani iliendelea kuwa wa pili katika darasa la takribani wanafunzi 128.

Nilimaliza kidato cha nne mwaka 2015 kwa ufaulu wa Div 1 ya point 14, nikiwa mwanafunzi wa kwanza kwa shule ambayo ilikuwa haina waalimu wa kutosha na mazingira duni sana.

Julai ya mwaka 2016 nilianza kidato cha tano katika shule ya Uwata boys high school iliyoko mbeya mjini. Nilisoma masomo yangu ya PCB mpaka mwaka 2018 ambapo nilimaliza masomo hayo nikiwa na ufaulu wa div 1 ya point 4.

Baada ya hapo nilienda jeshi la kujenga taifa (JKT) kikosi namba 825 KJ-MTABILA kigoma kwa mafunzo ya mujibu wa sheria, kuanzia june 2018 mpaka septemba 2018 miezi mitatu). Nilihudhuria mafunzo hayo katika OPARESHENI MERERANI mujibu wa sheria. 

November 2018, nilipokelewa chuo kikuu cha muhimbili na kupewa namba ya usajili 2018-04-12080, ambayo niliitumia kwa wakati wote nilipookuwa Chuko kikuu cgha Muhimbili kimasomo.

View profile

Comments (0)