Published - Wed, 28 Sep 2022
KUANGALIA MAJINA AU KUPATA PDF YA MAJINA BONYEZA LINK HII HAPA CHINI
BONYEZA KUPATA PDF YA MAJINA .
WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kesho inatarajia kutangaza majina ya wanafunzi 640 wanaostahili kupata ufadhili wa masomo kupitia Samia Scholarship baada ya kufanya vizuri masomo ya sayansi.
Waziri wa wizara hiyo, Profesa Adolf Mkenda alisema Jumapili jijini Dodoma kuwa katika kupata ufadhili huo hakutakuwa na upendeleo au ushawishi.
“Septemba 27, 2022 (kesho) tunafungua rasmi tangazo la wanafunzi waliomaliza kidato cha sita na kufanya mitihani kupitia Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) na kufaulu vizuri kwenye masomo ya sayansi ambao wanastahili kupewa Samia Scholarship, baada ya hapo majina yao yatatangazwa.” alisema Profesa Mkenda wakati wa kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu kufungua tangazo la Samia Scholarship.
Aliongeza “Kwa wanafunzi ambao wamefanya vizuri sana katika masomo ya sayansi ambao wanastahili kupewa Samia Scholarship tunayo majina 640, tutangaza.”
Profesa Mkenda alisema moja ya kigezo cha kupata ufadhili ni mwanafunzi kudahiliwa kwenye vyuo vikuu vya ndani ya nchi kusoma masomo ya sayansi, uhandisi na elimu tiba.
Alisema kwa mwanafunzi ambaye atadahiliwa kwenye masomo ambayo si ya sayansi hawatanufaika na ufadhili huo hata kama jina lipo kwenye orodha ya walio na sifa ya kupata.
“Unaweza ukawa umefaulu masomo ya sayansi na ukawemo kwenye orodha tutakayoitangaza lakini umeenda kwenda kusoma nje ya nchi kwa mtu anakusomesha basi utakosa fursa hii”alisema profesa Mkenda na kuongeza;
“Pia unaweza jina lako likawepo na umedahiliwa katika chuo kikuu hapa Tanzania nje ya masomo ya sayansi, uhandisi na elimu tiba utakosa fursa hiyo”
Aliongeza “Kikubwa mwanafunzi awe umefaulu masomo ya sayansi, hakuna lobbying matokeo ya nani kafauli vizuri yako wazi na kila mtu anaweza kuona, kwa hiyo hakuna cha kusema mtoto wa Mkenda au Silvia, hapana ulichofaulu ndio kitakufanya uchaguliwe.”
Profesa Mkenda alisema Wizara imetanga Sh bilioni tatu ambazo zinaweza kuwatosha wanafuzi 640 kwa mwaka wa kwanza.
“Tutakapoingia mwaka wa pili inaweza kuwa shilingi bilioni sita na zitaendelea kuongezeka kulingana na uhitaji, hapa tutazindua tangazo lakini uzinduzi wa hii scholarship yenyewe tumemuomba Rais akutane na hao watakaokuwa wamekamilisha vigezo vyote.”alisema.
Mimi ni mwanafunzi katika chuo kikuu cha MUST (Mbeya University Of Science And Technology), Ninasoma kozi ya Computer Engineering ngazi ya Degree. Mimi pia ni mbunifu wa mifumo ya kitehema kama vile www.drmlelwa.co.tz | www.webusiness.co.tz | www.sokoni.shop pia ipo mifumo ya hardware kama vile we-receiver, we-mixer na alama ya damu automation system na yote hii inafanya kazi na kutumiwa na watu. MOSTLY I LOVE GOD AND THE GOSPLE OF GOD
Safari yangu ya kielimu ilianza katika shule ya Msingi ya Ikulu iliyopo Ilomba jijini Mbeya, nilipomaliza nikaingia secondary katika shule ya Sekondari Pandahill Sec(2022 -2016), nikamalizia elimu yangu ya sekondari shule ya Jifunzeni sec iliyopo Hitua Mbeya(2017).
2018 nikaokoka(kanisa la KIKOSI KAZI CHA INJILI) na baada ya hapo nikaenda Morogoro na huu ndio ulikuwa mwanzo wa mabadiloko katika maisha yangu baada tu ya kuokoka nikapata akili kubwa mno sijawai ipata. 2020 nikiwa Kwiro Boys - PCM nikamaliza.
2020 Tukaanza kufundisha mimi na kaka yangu kupitia youtube BURE kabisa kama tulivyofundishwa ibadani. 2021 tulianza kuwatoza watu gharama kidogo ili tusilemewe.
Pia 2020 december nikaingia Must nikakutana watu wengine ujuzi nilionao ukaongezeka zaidi na 2022 nikaja na wazo hili la kutatua changamoto za kupata na kuuza ujuzi kwa njia ya Mtandao.
Dr Mlelwa litakuwa suruhisho la changamoto nyingi sana Tanzania kama watu watataka kuvuka katika changam,oto hizo.
Mungu awabariki wote
Mon, 02 Dec 2024
Sat, 07 Jan 2023
Thu, 01 Dec 2022
Write a public review